16. Kalenda za mahesabu juu ya kuandama kwa mwezi na kutumia darubini

Swali 16: Ni njia ipi ya Kishari´ah kwayo unathibiti kuanza kwa mwezi? Je, inafaa kutegemea hesabu za uchunguzi wa anga juu ya kuanza na kumalizika kwa mwezi? Je, inafaa kwa muislamu kutumia kile kinachoitwa “darubini” katika kuutafuta mwezi?

Jibu: Njia iliowekwa katika Shari´ah kuanza kwa mwezi ni watu kuona mwezi mwandamo. Hilo linatakiwa linatokana na ambaye kuna uaminifu juu ya dini na macho yake. Akiuona basi ni lazima kutenda kazi kwa mujibu wa uonaji huu ikiwa ni funga ya Ramadhaan na kufungua ikiwa mwezi mwandamo ni kwa ajili ya Shawwaal.

Haijuzu kutegemea hesabu za uchunguzi wa angani ikiwa si kwa njia ya kuona. Ikiwa watu watauona mwezi, hata kama ni kwa njia ya uchunguzi wa angani, basi ni wenye kuzingatiwa. Hayo ni kutokana na ueneaji wa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mkiuona, basi fungeni, na mkiuona fungueni.”[1]

Ama kuhesabu peke yake haijuzu kuifanyia kazi wala kuzitegemea.

Kuhusu kutumia kile kinachoitwa “darubini”, ambayo ni miwani inayovuta mwezi, hakuna neno. Lakini si lazima kufanya hivo. Kwa sababu udhahiri wa Sunnah unafahamisha watu kutegemea uonaji wa kawaida na si jengine. Lakini endapo darubini itatumiwa na akauona mwezi mtu ambaye anaaminiwa basi uonaji huo unatakiwa kufanyiwa kazi.

Watu hapo kale walikuwa wakitumia njia hiyo ambapo wanapanda juu ya minara katika usiku wa tarehe thelathini Sha´baan au katika usiku wa tarehe thelathini Ramadhaan ambapo wanautafuta kwa njia ya darubini hii. Kwa hali yoyote pale ambapo kutathibiti kuonekana kwa mwezi mwandamo – kwa njia yoyote ile itayotumiwa – basi ni lazima kufanyia kazi kwa mujibu wa uonaji huu. Hayo ni kutokana na ueneaji wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mkiuona, basi fungeni, na mkiuona fungueni.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1900) na Muslim (2471).

[2] al-Bukhaariy (1900) na Muslim (2471).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 18
  • Imechapishwa: 15/04/2021