96- Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitufunza Istikhaarah katika mambo yote kama anavyotufunza Suurah katika Qur-aan. Amesema: ”Mmoja wenu anapotaka kufanya jambo basi aswali Rakaa´ mbili mbali na Swalah ya faradhi na kisha aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخيرُكَ بِعِلْمِكَ وأَسْتَقْدِرُكَ بقدرَتِكَ وأَسْأَلُكَ منْ فَضْلِكَ الْعَظِيمِ فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أَقْدِرُ وَتَعْلَمُ وَلاَ أَعْلَمُ وَأَنْتَ عَلاَّمُ الْغُيُوبِ اللهُمَّ إِنْ كُنتَ تَعلم أَنَّ هذَا الأَمْرَ خيرٌ لِي في دِيني وَمَعَاشي وَعاقِبة أَمْرِي وَعَاجِلِهِ وَآجِلِهِ فاقْدُرْهُ لِي وَيَسِّرْهُ لي ثمَّ بَارِكْ لي فيهِ وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَم أَنَّ هَذا الأَمْرَ شَرٌّ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي وَعَاجِلِهِ وَآجِلِهِ فاصْرِفْهُ عَنِّي واصرفْنِي عَنْهُ واقْدُرْ لِيَ الْخَيْرَ حَيْثُ كانَ ثم رضِّنِي بهِ

“Ee Allaah! Hakika mimi ninakutaka kwa ujuzi Wako na ninakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako. Ninakuomba kwa fadhila Zako kubwa. Hakika Wewe unaweza na mimi siwezi. Wewe unajua na mimi sijui. Wewe ni Mjuzi wa yale yaliyofichikana. Ee Allaah! Endapo unajua kuwa jambo hili – litaje jambo lako – ni kheri kwangu katika Dini yangu, mwisho wa maisha yangu duniani na Aakhirah, basi nakuomba uniwezeshe na unisahilishie, kisha nibariki kwalo. Na endapo unajua kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu, mwisho wa maisha yangu duniani na Aakhirah, basi nakuomba liepushe na mimi na mimi uniepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri na mimi popote lilipo, halafu niridhishe kwalo.”

Anayemuomba Muumba ushauri na akawashauri viumbe hatojuta hatojuta. Badala yake atakuwa ni mwenye uthabiti juu ya jambo lake. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ

“Na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali.” (Aal ´Imraan 03 : 159)

Qataadah amesema:

”Hakuna watu watakaotaka ushauri wengine wakikusudia kupata ujira wa Allaah isipokuwa wataongozwa kwa yale ambayo ni kheri kwao.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 68-70
  • Imechapishwa: 21/03/2017