16. Ibn Baaz kuhusu mgonjwa kutibiwa na daktari wa jinsia nyingine

Swali 16: Unasemaje juu ya daktari wa meno mwanaume kumtibu mwanamke? Inajuzu kufanya hivo pamoja na kuzingatia kwamba madaktari wa meno wanaume wamejaa katika kitengo na nchi hiyohiyo?

Jibu: Tumejaribu na kufanya kazi mara nyingi tukishirikiana na wahusika ili kuwepo matibabu ya wanaume kwa wanaume na matibabu ya wanawake kwa wanawake na wanaume wawatibu wanaume wenzao na wanawake wawatibu wanawake wenzao kuhusiana na meno na mengineyo. Hivi ndio usawa.  Kwa sababu mwanamke ni ´Awrah na fitina isipokuwa wale waliorehemewa na Allaah.

Ni lazima kuwepo madaktari wataalam wa kike kwa wanawake na madaktari wataalam wa kiume kwa wanawake. Isipokuwa tu wakati wa dharurah kubwa. Kwa mfano mwanaume akipatwa na maradhi yasiyoweza kutibu daktari wa kiume. Katika hali hii hakuna neno. Allaah amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“… na ilhali ameshakubainishieni yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.”[1]

Vinginevyo ni lazima kuwepo kwa madaktari kwa wanaume na madaktari kwa wanawake. Jengine kitengo cha madaktari wa kiume kiwe upande wake na kitengo cha madaktari wa kike kiwe upande wake. Vilevile kuna uwezekano kukawa hospitali maalum kwa ajili ya wanawake na hospitali maalum kwa ajili ya wanaume ili kila mtu aweze kuepukana na fitina na mchanganyiko wenye kudhuru. Hili ndio jambo la wajibu kwa kila mmoja.

[1] 06:119

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 18/07/2019