698- Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Masiku yatafufuliwa kwa muonekano wake na huku siku ya ijumaa itafufuliwa ikiwa ni yenye kung´ara na kuangaza. Watu wake wataizunguka kama harusi inayopelekwa chumbani kwake. Itawaangazia na watatembea katika mwanga wake. Rangi zao zitakuwa kama theluji nyeupe na watakuwa na harufu kama ya miski. Watatembea katika jibali ya kafuri na viumbe watawatazama. Hawatoshusha macho yao chini kwa sababu ya kushangazwa mpaka waingie Peponi. Hakuna atayechanganyikana nao isipokuwa wale waadhini wenye kutarajia malipo kutoka kwa Allaah.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy na Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” yake na akasema:

”Endapo mapokezi haya yatakuwa Swahiyh. Ndani ya nafsi yangu kuna kitu juu ya mlolongo wa wapokezi huu.”

Haafidhw amesema:

”Mlolongo wa wapokezi wake ni mzuri na matini yake ni geni.”

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/437)
  • Imechapishwa: 13/01/2018