16. Dalili ya kumi na nne kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


14- Shaykh Abul-Fath Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy´ aliuweka mkono wake juu ya bega langu na  akatukhabarisha: Abu ´Abdillaah Muhammad bin Abiy Naswr al-Humaydiy aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: Abu Ishaaq Ibraahiym bin Sa´iyd bin ´Abdillaah an-Nu´maaniy aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: Abu Sa´d Ahmad bin Muhammad bin Ahmad aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: Abul-Hasan Ahmad bin ´Iysaa al-Faradhiy aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: Abul-Hasan Ahmad bin al-Hasan bin Muhammad al-Makkiy aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: Abu ´Amr Hilaal bin al-´Alaa’ ar-Raqqiy aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: Baba yangu aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akanihadithia: Abu Ishaaq as-Sabiy´iy aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: ´Abdullaah bin al-Haarith aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akanihadithia: al-Haarith al-A´war aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akanihadithia: ´Aliy bin Abiy Twaalib aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akatuhadithia: Mtume wa Allaah aliuweka mkono wake juu ya bega langu na akanihadithia:

“Mkweli, mtamkaji, mjumbe wa Mola wa walimwengu na ambaye ni mwaminifu juu ya Wahy Wake Jibriyl aliuweka mkono wake juu ya beg langu na akanihadithia: Nimemsikia Israafiyl akisema: Nimeisikia kalamu ikisema: Nimesikia Ubao ukisema: Nimemsikia Allaah (Ta´ala) akiwa juu ya ´Arshi akikiambia kitu “Kuwa!” na kikawa. Hawahi kutamka neno lote isipokuwa kinakuwa.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 90-91
  • Imechapishwa: 02/06/2018