16. Dalili juu ya mkono wa Allaah 2

16- Abu Twaalib al-Haafidhw Ahmad bin Naswr bin Twaalib ametuhadithia: Sulaymaan bin ´Abdil-Hamiyd bin Sulaymaan Abu Ayyuub al-Bahraaniy ametuhadithia kutoka kwenye kitabu chake: Abu Sulaymaan ´Utbah bin as-Sakan al-Fazaariy ametuhadithia: Artwa´ah bin Mundhir ametuhadithia: Layth bin Abiy Sulaym ametuhadithia, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu cha kwanza alichoumba Allaah (´Azza wa Jall) ni kalamu. Akaichukua kwa mkono Wake wa kuume – na mikono Yake yote miwili ni ya kuume – na akaandika kila kitachokuwa katika matendo mema na maovu, kilichorutubika na kikavu. Akakichukua Kwake katika kumbukumbu. Kama mnataka msome:

هَـٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Hiki kitabu Chetu kinatamka juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika yale mliyokuwa mkiyatenda.” [1]

Ni kipi chenye kuandikwa kama si kitu ambacho tayari kimeshapangwa?”[2]

[1] 45:29

[2] Ibn Abiy ´Aaswim (107) na ash-Shariy´ah, uk. 187, ya al-Aajurriy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 05/11/2017