159. Muhalalishieni ndugu yenu?


Swali 159: Ni ipi hukumu ya maneno ya wafiwa wa maiti kuwaambia watu:

“Mfanyieni halali ndugu yenu.”

na pia kuwaambia wamwombee msamaha[1]?

Jibu: Sijui msingi wa jambo hilo. Lakini ni sawa ikiwa anajua kuwa ni amewadhulumu na akawaomba wamhalalishie. Vinginevyo atosheke na kuwaomba wamwombee du´aa na msamaha.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/409).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 116-117
  • Imechapishwa: 22/01/2022