Swali 157: Ni ipi hukumu ya maneno yao wakati wa tanzia:

“Ameenda katika mahali pake pa mwisho pa kupumzikia.”[1]?

Jibu: Sitambui ubaya wa kusema hivo. Kwa sababu ni mahali pake pa mwisho kwa nisba ya ulimwenguni. Ni neno la watu wasiokuwa na elimu. Ukweli wa mambo ni kwamba pahali pa mwisho ni Pepo ambayo ni kwa ajili ya wenye kumcha Allaah na Moto kwa ajili ya makafiri.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/408-409).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 116
  • Imechapishwa: 22/01/2022