Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

2- Yule mwenye kuabudiwa hali ya kuwa yuko radhi kwa hilo.

MAELEZO

Bi maana ameabudiwa hali ya kuridhia watu wamwabudu. Huyu ni Twaaghuut. Kuhusu mwenye kuabudiwa hali ya kuwa hayuko radhi kwa hilo haingii katika hili. Kwa sababu ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameabudiwa badala ya Allaah lakini si mwenye kuridhia jambo hilo. Isitoshe mama yake, ´Uzayr, mawalii na waja wema wengine wa Allaah si wenye kuridhia jambo hilo. Bali walikuwa ni wenye kukemea jambo hilo na wakimpiga vita mwenye kulifanya. Kwa hiyo yule mwenye kuabudiwa na hayuko radhi kwa jambo hilo haitwi kuwa ni Twaaghuut. Kwa ajili hiyo wakati Allaah alipoteremsha:

إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ

”Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni mawakio ya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia.”[1]

Washirikina wakafurahi na wakasema kuwa wao wanamwabudu al-Masiyh na wengineo. Kwa hiyo watakuwa pamoja nao Motoni. Hapo ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha:

إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَـٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِي مَا اشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَالِدُونَ

“Hakika wale ambao umewatangulia wema Wetu, basi hao watatenganishwa nao; hawatosikia mvumo wake nao watadumu katika ambayo zimetamani  nafsi zao.”[2]

Katika Aayah nyingine walisema:

وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ

“Wakasema: “Je, waabudiwa wetu ni bora au yeye?”[3]

Wakimaanisha ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kisha akasema:

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ

”Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka ubishi. Bali wao ni watu makhasimu. Yeye [Nabii ´Iysaa] si chochote isipokuwa tu ni mja tuliyemneemesha na tukamfanya ni mfano kwa wana wa israaiyl.”[4]

Yeye ni mja wa Allaah na hayuko radhi kuabudiwa badala ya Allaah. Bali Allaah amemtumiliza kukaripia jambo hilo:

مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ

”Sijawaambia isipokuwa yale uliyoniamrisha kwayo kwamba: ”Mwabuduni Allaah, Mola wangu na Mola wenu.”[5]

Yule mwenye kuabudiwa hali ya kuwa si mwenye kuridhia hilo haingii ndani ya makemeo hayo. Haingii ndani ya makemeo haya na wala hawi Twaaghuut. Kwa sababu ni mwenye kukemea jambo hilo. Kwa sababu Twaaghuut ni yule mwenye kuridhia kuabudiwa badala ya Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 21:98

[2] 21:101-102

[3] 43:58

[4] 43:58-59

[5] 05:117

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 300-302
  • Imechapishwa: 23/02/2021