154. Mambo ya ukumbusho anayofanyiwa maiti

Swali 154: Ni wapi limetokea jambo la ukumbusho (الذكرى) analofanyiwa maiti siku ya tatu tangu pale alipowekwa ndani ya kaburi[1]?

Jibu: Limezuliwa ni wajinga juu ya Uislamu na yale yanayowapasa kufanya katika kuhifadhi misingi na matawi yake. Hawana uzani wowote wa kidini uliosalimika. Bali wamepachikwa kuwaigiliza wapotofu. Kwa hiyo ni Bid´ah iliyozuliwa ndani ya Uislamu. Kwa hiyo inakuwa ni yenye kurudishwa nyuma kwa mujibu wa Shari´ah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/398).

[2] Muslim (1718).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 27/01/2022