151. Ibn-ul-Qayyim kuhusu aina mbalimbali ya Twawaaghiyt


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Twaaghuut ni kila chenye kuabudiwa, kinachofuatwa au kutiiwa ambacho mja anapindukia mipaka yake.”

MAELEZO

Kuhusu maana ya Twaaghuut kwa mujibu wa Shari´ah ni kama alivosema Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) na Shaykh akamnakili hapa. Twaaghuut ni kile ambacho mja anapinduka kwacho mpaka. Mja na mipaka kwa sababu yeye ni mja. Allaah amemwekea mipaka. Kwa hiyo ni lazima kwake kusimama katika mipaka hiyo. Akiivuka basi anakuwa Twaaghuut. Akiivuka mipaka ya Allaah ambayo Allaah amewawekea waja Wake na akawaamrisha wasiivuke na wasiikurubie basi huyo ni Twaaghuut. Akimwasi Allaah, akaivuka mipaka Yake na akapindukia anaitwa Twaaghuut. Kwa sababu amepindukia na kuivuka mipaka ya Allaah. Maneno yake:

”Twaaghuut ni kila chenye kuabudiwa, kinachofuatwa au kutiiwa ambacho mja anapindukia mipaka yake.”

Hii ndio maana yenye kuenea ya Twaaghuut. Kwa sababu Allaah ameamrisha kumwabudu Yeye pekee hali ya kuwa hana mshirika, vilevile akaamrisha kumfuata Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akaamrisha kumtii Yeye na kumtii Mtume Wake katika aliyohalalisha na aliyoharamisha. Mwenye kuvuka mpaka huu ni Twaaghuut. Mwenye kuvuka mpaka wa ´ibaadah ambao ameuwajibisha, akaufanya ni maalum Kwake na kuukanusha kwa mwengine ambapo akamwabudu Allaah pamoja na wengine ni Twaaghuut. Mshirikina ni Twaaghuut. Kwa sababu amevuka mpaka katika ´ibaadah na akawaabudu wengine pamoja na Allaah. Amemwelekezea ´ibaadah mwengine asiyestahiki.

Vivyo hivyo inahusiana na mwenye kuabudiwa hali ya kuwa ni mwenye kuridhia hilo. Yule ambaye anaabudiwa na Allaah, akafurahia na akajikweza kwa jambo hilo huyo ni Twaaghuut. Mfano wa Fir´awn, Namruud na Mashaykh wa Suufiyyah waliochupa mpaka ambao wanaabudiwa na wafuasi wao na wakaridhia jambo hilo au wakawalingania watu wawabudu, kama itavyokuja huko mbele. Huyu ni Twaaghuut katika ´ibaadah.

Maneno yake:

”… au kinachofuatwa

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewaamrisha viumbe wote kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijuzu kwa yeyote kumfuata asiyekuwa yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ambaye atamfuata asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akadai kuwa kitendo hicho kinafaa basi mtu huyo ni Twaaghuut. Kwa vile atakuwa amemfuata asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye kumeamrishwa kumfuata. Kufuata ni jambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama wengineo katika wanachuoni na walinganizi wanafuatwa pindi watapofuata mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anayestahiki kufuatwa ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa wengine ni wafikishaji peke yake. Wanafuatwa kwa yale ya haki na kwa yale waliyoafikiana kwayo kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijuzu kuwafuata kwa yale wanayokwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano wa hilo ni Mashaykh wa Suufiyyah ambao wanafuatwa na wale muridi wao na waja wao katika yale yasiyokuwa utiifu kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali wanasema kuwa hawana haja ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanasema kuwa wao wanachota kule alikochota Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba wanapokea moja kwa moja kutoka kwa Allaah! Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapokea kutoka kwa Allaah kupitia uunganishi wa Jibriyl na kwamba wao wanapokea moja kwa moja kutoka kwa Allaah. Pia wanasema kuwa sisi tunaipokea dini yetu kutoka kwa mfu na kwamba wao wanaipokea dini yao kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa sababu wanadai kuwa Mashaykh zao wanawasiliana na Allaah na wanapokea moja kwa moja kutoka kwa Allaah. Kiwango kimewafikisha katika ukafiri huo. Huo ndio mfumo wao. Hapana shaka kwamba hao ndio viongozi wa Twawaaghiyt.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 295-298
  • Imechapishwa: 22/02/2021