151. Anayekataa kujifunza elimu na kuitendea kazi

Wale ambao wamechukua elimu wakaacha matendo ndio wale:

الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ

“Walioghadhibikiwa.” (al-Faatihah 01:07)

miongoni mwa mayahudi na waliowafuata katika wale waliojifunza dini ya Allaah, lakini hata hivyo hawakuifanyia kazi. Na wale waliolazimiana na matendo na wakaacha elimu, hawa ndio manaswara na walioafikiana nao katika wafanya ´ibaadah na Suufiyyah ambao wanamuabudu Allaah kwa ujinga na upotevu na hawataki elimu. Wanasema kwamba elimu inakinzana na matendo. Wakati mwingine wanasema ukifanya matendo, basi elimu itakujia yenyewe bila ya kujifunza na kwamba utafunguliwa kifua chako bila ya wewe kujifunza kwa wanachuoni. Hivi ndivo wanavyoona Suufiyyah tokea hapo zamani mpaka sasa. Wanapuuza kujifunza elimu, kukaa kwa wanachuoni na wanasema kinachotakikana ni matendo tu na kwamba eti utapofanya matendo na ukamuabudu Allaah, basi Allaah atakufungulia elimu bila ya wewe kujifunza. Huu ni upotevu.

Yule anayekataa kujifunza elimu kwa kuipuuza ni kafiri. Yule anayeyakataa matendo kabisa pia anazingatiwa ni kafiri. Kwa ajili Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuipuuza dini ya Allaah; hajifunzi nayo na wala haifanyii kazi.”

Hajifunzi nayo, hii ndio njia ya:

الضَّالِّينَ

“Waliopotea.” (al-Faatihah 01:07)

Katika manaswara, Suufiyyah na wengineo.

Na wala haifanyii kazi, hii ndio njia ya mayahudi na waliofuata njia yao miongoni mwa kila mwanachuoni ambaye haifanyii kazi elimu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 191
  • Imechapishwa: 14/03/2019