Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah amewafaradhishia viumbe vyote kukanusha Twaaghuut na badala yake kumuamini Allaah.

MAELEZO

Allaah amewafaradhishia viumbe… – Kisha akataja maana ya Twaaghuut. Twaaghuut Allaah ameitaja katika Aayah nyingi ikiwa ni pamoja na zifuatazo:

فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

”Basi yule atakayemkanusha Twaaghuut na akamuamini Allaah, basi hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia, Mjuzi. Allaah ni mlinzi wa wale walioamini; anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru na wale waliokufuru marafiki wao ni Twaaghuut; huwatoa kutoka katika nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa Motoni wao humo watakuwa ni wenye kudumu.”[1]

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا

“Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini masanamu na Twaaghuut na wanasema juu ya wale waliokufuru “Wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.””[2]

Aayah hii imeteremka juu ya mayahudi.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut ilihali wameamrishwa wakanushe hiyo.”[3]

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.””

Neno Twaaghuut limechukuliwa kutoka katika Twughyaan. Maana yake ni kuchupa mipaka. Kunasemwa kuwa maji yamepinduka mpaka (طغى الماء) pindi yanapopanda kiwango chake. Amesema (Ta´ala):

إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ

”Hakika Sisi, pale maji yalipopinduka mipaka, tulikubebeni katika merikebu.”[4]

[1] 02:256-257

[2] 04:51

[3] 04:60

[4] 69:11

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 294-295
  • Imechapishwa: 22/02/2021