15. Washirikina wa leo ni waovu zaidi kuliko wale wa kale

Washirikina waliokuja nyuma wamewashinda wale washirikina wa kale kwa njia mbili:

1 – Baadhi yao wameshirikisha katika uola wa Allaah.

2 – Wanashirikisha katika kipindi cha raha na shida.

Hayo yanatambulika na wale waliochanganyika nao, wakazisoma hali zao na wakaona yale wanayoyafanya kwenye kaburi la al-Husayn, al-Badawiy na wengineo waliyoko huko Misri, kwenye kaburi la al-´Aydaruus huko Aden, al-Haadiy huko Yemen, Ibn ´Arabiy huko Shaam, Shaykh ´Abdul-Qaadir al-Jaylaaniy huko ´Iraaq na makaburi mengine yanayojulikana ambayo wajinga wameyapindukia mpaka kwa kuyafanyia mengi ambayo ni haki ya Allaah (´Azza wa Jall). Watu hawa wanatakiwa kukaripiwa na kubainishiwa Tawhiyd ya hakika ambayo Allaah amemtuma nayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Mitume waliokuwa kabla yake (´alayhim-us-Swalaatu was-Sallaam). Tunamuomba Allaah awarudishe katika uongofu wao, afanye kuwepo kati yao walinganizi wengi wa uongofu na awawafikishe wanachuoni wa waislamu waweze kupambana na shirki hii na waitokomeze na vilevile watokomeze njia zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na yukaribu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 13
  • Imechapishwa: 31/05/2023