15. Wametilia bidii katika Anaashiyd


15- Pote la al-Ikhwaan al-Muslimuun linapindukia kwa Anaashiyd (أناشيد) na Qaswiydah na kutilia nguvu katika kuzihifadhi na kuzisikiza kwa hali ya khatari. Baadhi yazo zimeambatana na ala za muziki kama ngoma. Wamezipanga kwa njia mbalimbali. Wanasema:

“Ni Anaashiyd za Kiislamu. Anayepingana nazo haelewi kabisa mambo ya kisasa.”

Kuna waimbaji, wanaojinasibisha na kundi limoja la Kiislamu, alinambia:

“Ninawaimbia watu Anaashiyd mpaka wanaanza kulia.”[1]

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 21
  • Imechapishwa: 25/03/2017