15. Wajibu tu ndio iwezayo kuitikisa wajibu nyingine

6- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Wapanda farasi wanaume walikuwa wakitupitia na sisi tuko kwenye Ihraam pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanapotujongelea, kila mmoja wetu anateremsha mavazi yake ya juu, Jilbaab, usoni mwake. Wanapokuwa wameshapita, tunajifunua tena.”[1]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na Ibn Maajah.

Katika maneno yake “Wanapokuwa wameshapita, tunajifunua tena” kuna dalili yenye kuonesha kuwa ni wajibu kufunika uso. Kwa sababu imewekwa katika Shari´ah kufunua uso katika Ihraam. Lau kusingelikuwepo kizuizi kikubwa kungelibaki kuwa ni wajibu kuufunua uso. Mwanamke kufunua uso katika Ihraam ni wajibu kwa mujibu wa wanachuoni wengi. Lililo la wajibu linaweza kutikiswa tu na la wajibu lingine. Lau isingelikuwa ni wajibu kufunika uso mbele ya wanaume ajinabi, basi isingeliruhusiwa kuufunika katika Ihraam. Imethibiti katika al-Bukhaariy, Muslim na wengine ya kuwa hairuhusiwi kwa mwanamke mwenye kuhirimia kuvaa Niqaab wala vifuniko vya mikono[2]. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hili linaonyesha kuwa Niqaab na vifuniko vya mikono ilikuwa ni mambo yenye kujulikana kwa wanawake mbali na Ihraam, jambo lenye kupelekea kufunika nyuso zao na mikono yao.”[3]

Dalili hizi sita ni zenye kuonesha kuwa ni wajibu kwa mwanamke kujisitiri na kufunika uso wake mbele ya wanaume ajinabi. Tukiongezea juu yake na zile dalili nne za Qur-aan inakuwa dalili kumi.

[1] Ahmad (24522).

[2] al-Bukhaariy (1838).

[3] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/276).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 19-21
  • Imechapishwa: 26/03/2017