[22] Kiumbe bora baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ambaye ana manzilah ya juu kabisa baada ya Manabii na Mitume na ambaye ana haki zaidi ya ukhaliyfah baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh). Baada ya hapo anafuatia ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh). Halafu anafuatia Dhun-Nuurayn ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh). Kisha anafuatia Abul-Hasan ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh).

Tunawashuhudilia wale kumi Pepo ambao ni Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, Sa´d, Sa´iyd, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah. Mtu anatakiwa kumuomba Allaah awarehemu Maswahabah wote wa Mtume wa Allaah, kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao, na pia kuyataja mazuri yao.

Mu´aawiyah ndiye mjomba wa Waumini na alikuwa ni mwandishi wa Wahy wa Mola wa walimwengu.

  • Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 27/02/2019