15. Ni ipi hukumu mfungaji kula na kunywa kwa kusahau?

Swali 15: Ni ipi hukumu iwapo mfungaji atapitikiwa na kula na kunywa kwa kusahau?

Jibu: Swawm haikatiki mfungaji akipitikiwa na kula na kunywa kwa kusahau. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kula na kunywa kwa kusahau ilihali amefunga, atimize swawm yake. Hakika  si mwengine ni Allaah ndiye kamilisha na kumnywesha.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1933) na Muslim (1155).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 31
  • Imechapishwa: 12/06/2017