Sayyid Qutwub anazungumza kwa ujamaa na kutokomeza utumwa, jambo ambalo ni utungaji Shari´ah. Katika hayo kunaingia vilevile maoni yake ya mwisho, ya kijamaa aliyoyathibitisha katika “al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah”, “Ma´rakat-ul-Islaam war-Ra´smaaliyyah” na “as-Salaam al-´Aalamiy”. Shaykh Bakr hakutaja maneno yake kutokana na sababu mbili:

1- Wingi wake.

2- Baada tu karibuni niliandika mlango mpya maalum ambapo nilifuatilia fikira za ujamaa za Sayyid Qutwub.

Katika vifungu vilivyoashiriwa kuna vifungu ambavyo nimebainisha namna ambavyo Sayyid Qutwub anajuzisha uwekaji Shari´ah unaotokomeza utumwa na kwamba inajuzu kwa ulimwengu kutambua mpangilio mwingine. Nilieleza namna ambavyo Sayyid Qutwub anathibitisha utungaji kanuni huu katika “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan”, sehemu nne katika tafsiri ya “al-Baqarah”, “at-Tawbah”, “al-Mu´minuun” na “Muhamamd”. Nilirejesha nukuu zote hizi katika vyanzo vya hashiya ya kitabu. Hii ni ibara tu ya kitabu kingine mbali na “al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah” kwa yule mwenye kufahamu na akawa na inswafu. Ni vipi Shaykh Bakr anaweza kuthubutu kusema kuwa hakupata isipokuwa nukuu moja tu kutoka katika “al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah”. Baada ya hapo anafanya jambo kuwa baya zaidi kwa kutotaja nukuu anayoikosoa.