Kuna uandishi mwingine pia. Kwa mfano waandishi watukufu wanaandika yale yote tunayoyafanya kwa kukopi yale yaliyomo kwenye Ubao uliohifadhiwa. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

هَـٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Hiki kitabu Chetu kinatamka juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika yale mliyokuwa mkiyatenda.” [1]

Uandikwaji unatokana na kitu ambayo tayari kimeshaandikwa, nacho ni Ubao uliohifadhiwa ambao Allaah amesema juu yake:

إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ

“Hakika Sisi tunahuisha wafu na tunaandika yale waliyoyatanguliza na athari zao na kila kitu tumekirekodi barabara katika kitabu kinachoweka wazi.”[2]

Kadhalika yale yanayoandikwa kila mwaka katika usiku wa Qadar; hali na mambo ya watu, muda wa watu kuishi, ajali, furaha, uhai, kifo, ufukara, utajiri, woga, amani, wema, shari na kadhalika. Hakuna kinachotofautiana na yale yaliyomo kwenye Ubao uliohifadhiwa; yote haya ni yenye kuafikiana nayo.

Kwa hivyo ni lazima kuamini Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh), Hadiyth ya kuhusu uonekanaji, Qadar na kadhalika, ni mamoja mtu amefahamu maana yake au hakufahamu maana yake. Kufahamu maana yake ni nuru juu ya nuru. Yule asiyefahamu maana yake aulize. Wanachuoni wenye upeo wapo na himdi zote anastahiki Allaah. Japokuwa mtu atalazimika kusafiri kwa ajili ya kuuliza juu ya jambo hili kubwa la ´Aqiydah kuna faida. Nguzo zote sita za imani na mfano wake ni katika mambo yanayohusu ´Aqiydah. Katika hayo ni kuamini Qadar na kwamba kheri na shari yote yamekadiriwa na Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Hayatakiwi kufanyiwa kipingamizi, kudangana, kutoshika msimamo wowote wala kusita; bali inatakiwa kuamini, kusadikisha, kujisalimisha na maamrisho ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na moyo uwe ni wenye yakini kama mlima imara.

[1] 45:29

[2] 36:12

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 66
  • Imechapishwa: 07/10/2019