15. Magaidi Saudi Arabia daima huishilia wakiwa watwevu

Ugaidi kwa mujibu wa istilahi zake zote ni maradhi yenye kuua, tabia yenye kukemewa na janga kubwa lililoupata ulimwengu mzima. Katika kila nchi una sura yake, malengo yake, athari yake na dawa yake kutegemea na kanuni za nchi yenyewe, nidhamu zake, desturi zake, mila zake, Uislamu, tabia zake na maadili yake.

Hapa nitatosheka na kuandika mfumo wa namna ya kutibu ugaidi na ni nani mwenye jukumu la kuutunza ugaidi huo.

Kabla ya kuingia katika maudhui haya nataka kukumbusha jambo moja linalotambulika na kila mmoja. Hakuna watu wa matamanio wahusika wa tabia mbovu wanaosababisha aina yoyote ya ugaidi nchini Saudi Arabia isipokuwa Allaah huifanya nchi na raia wake kushinda na magaidi kudhalilika kubaya kabisa. Yale mashambulizi ya kigaidi yaliyotangulia ni ushahidi bora kabisa wa haya niyasemayo.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 22
  • Imechapishwa: 14/04/2017