15. Kuoga kabla ya kulala ndio bora zaidi


13- Kuoga kabla ya kulala ndio bora zaidi

Kuoga kabla ya kulala ndio bora zaidi kutokana na Hadiyth ya ´Abdullaah bin Qays aliyesema:

“Nilimuuliza ´Aaishah kwa kusema: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya vipi katika janaba? Je, alikuwa akioga kabla ya kulala au akilala kabla ya kuoga?” Akajibu: “Alikuwa akifanya yote hayo; wakati fulani alikuwa akioga kisha ndio analala na wakati mwingine akitawadha ndio analala.” Ndipo nikasema: “Himdi zote anastahiki Allaah ambaye amejaalia wasaa katika jambo hili.”[1]

[1] Ameipokea Muslim (01/171), Abu ´Awaanah (01/278) na Ahmad (06/73) na (149).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 117-119
  • Imechapishwa: 10/03/2018