Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kundi lililookoka liko kati na kati katika mlango wa matendo ya Allaah… “

Limeitwa “lililookoka” kwa sababu limeokoka kutokamana na Moto. Tofauti na mapote mengine ambayo yako Motoni. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ummah huu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu. ”

Hili limoja ndio lililookoka kutokamana na Moto. Makundi haya ya Motoni yanatofautiana. Miongoni mwayo yako yaliyoingia Motoni kwa sababu ya ukafiri na hivyo yatadumishwa humo milele. Miongoni mwayo yako yaliyoingia Motoni kwa sababu ya madhambi yake na hivyo hayatodumishwa humo milele. Kwa hiyo haina maana kwamba mapote yote haya ni ya kikafiri. Bali ni yenye kutofautiana. Kwa sababu tofauti inatofautiana. Maneno yake:

“… baina ya Qadariyyah na Jabriyyah.”

Jabriyyah ni wafuasi wa al-Jahm bin Swafwaan ambaye ana imani ya kutenzwa nguvu (الجبر), imani ya Irjaa´ (لإرجاء) na imani ya kupinga majina na sifa za Allaah (التجهم). Kwa ajili hiyo Ibn-ul-Qayyim amesema katika “an-Nuuniyyah” yake:

Jiym na jiym kisha akakusanya jimaa pamoja na mbili hizo

zikaambatana na herufi za mizani

Bi maana amekusanya kati ya jiym tatu na jiym ya nne ni Moto wa Jahannam – tunaomba Allaah atulinde nao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 08/03/2021