Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakaa baadhi ya siku Qubaa´. Maoni mengine yanasema kuwa alikaa siku kumi na nne. Huko ndio akaasisi msingi wa Qubaa´. Baada ya hapo akaendelea na safari yake kwa maamrisho ya Allaah (Ta´ala). Ilikuwa ni siku ya Ijumaa ndio alifika kwa Banuu Saalim bin ´Awf. Akaswali swalah ya Ijumaa kwenye msikiti wa Raanuunaa bondeni. Watu wa kabila wakamuomba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aishi kati yao, akasema:

“Iacheni ngamia. Hakika ni yenye kuamrishwa.”[1]

Wakati ilipofika mahali ambapo msikiti wake upo hii leo, ikapiga magoti. Hakuteremka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka pale ilipoinuka tena, ikapiga tambo kidogo, ikageuka kisha ikapiga magoti ile sehemu ya kwanza ilipoanda kupiga magoti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akashuka. Ilikuwa kwa Banuun-Najjaar. Abu Ayyuub akabeba mabegi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nyumbani kwake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanunua ardhi ya msikiti. Hapo kabla ilikuwa ni mahali pa mayatima wawili wanapofugia ngamia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya sehemu hiyo kuwa msikiti na ndio msikiti wake hii leo. Karibu yake akajenga nyumba ya wake zake.

Kuhusiana na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) alibaki Makkah ili kurudisha nafasi za watu walizokuwa nazo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mambo mengine. Kisha baada ya hapo na yeye akajiunga na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bayhaqiy katika ”Dalaa-il-un-Nubuwwah” (2/508). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”adh-Dhwa´iyfah” (6508).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 18/03/2017