4- Kufanya chuku. Ni kule kutoa damu kwenye ngozi pasi na mishipa. Pale ambapo mfungaji ataumikwa basi swawm yake imeharibika. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”[1]

Pia swawm ya yule aliyemfanyia inaharibika. Isipokuwa ikiwa atamfanyia chuku kwa kifaa kilichojitenga na asihitajie kugusa damu. Basi katika hali hiyo haiharibiki – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

Kitu kingine kilicho na maana ya kufanya chuku ni kutoa damu kwenye mishipa kwa ajili ya kupeana.

Ama kutokwa na damu kwenye donda, kung´oa jino au kutokwa na damu puani ni jambo lisilodhuru. Kwa sababu sio kufanya chuku na wala haina maana ya kuumikwa.

[1] Abu Daawuud (2367), Ibn Khuzaymah (1983). al-Albaaniy amesahihisha cheni ya wapokezi wake. Tazama “at-Ta´liyq ´alaa Ibn Khuzaymah” (03/236).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 158
  • Imechapishwa: 25/04/2020