15. Idadi ya siku za Ramadhaan


Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ

Na ili mkamilishe idadi [katika wakati wake uliyowekwa].”[1]

Allaah (´Azza wa Jall) anaamrisha kukamilisha idadi. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkifunikwa na mawingu basi timizeni idadi ya siku thelathini.”

Ina maana kwamba iwapo waislamu hawatoona mwezi mwandamo, basi wanachotakiwa ni wao kukamilisha Sha´baan siku thelathini. Haijuzu kufanya mwezi ukawa siku ishirini na tisa bila dalili. Lakini haina shaka kwamba mwezi unaweza kuwa siku ishirini na tisa, lakini mwezi unaofuata unaanza pale mwezi mwandamo unapoonekana. Tusipoona mwezi mwandamo basi ni lazima kukamilisha mwezi tuliopo sasa siku thelathini.

[1] 02:185

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 27
  • Imechapishwa: 02/06/2017