15. Haijuzu kwa mlezi kunyanyua mikono juu na kufuata wengine wanavofanya

Haifai kwa mwanamke akajisalimisha na hali ilivyo sasa na akasema kuwa watu wote wamekuwa juu ya jambo hilo na kwamba yeye hawezi kubadilisha kitu. Lau tungelibaki namna hii wenye kujisalimisha na hali ya sas ilivyo basi yasingelipatikana marekebisho. Marekebisho ni lazima kubadilisha yale yaliyoharibika kwa njia iliyokuwa nzuri. Ni lazima vilevile kubadilisha kilicho kizuri kwenda kwa kilicho kizuri zaidi mpaka mambo yatengemae.

Mtu kujisalimisha na hali ya kisasa ni jambo ambalo halikuthibiti katika Shari´ah ya Uislamu. Kwa ajili hii pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotumwa kwa watu washirikina ambao wanayaabudu masanamu, wanakata kizazi na wanawadhulumu na kuwanyanyasa watu pasi na haki hakujisalimisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali Allaah (´Azza wa Jall) hakumpa idhini ya kujisalimisha na hali iliyopo sasa. Alimwambia (Subhaanah):

فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ

“Basi tangaza wazi yale uliyoamrishwa na jitenge mbali na washirikina.”[1]

Akamwamrisha (Subhaanah) kuzungumza haki, kuwapeuka wajinga, kupuuza ujinga na uadui wao ili aweze kufikia malengo, jambo ambalo lilitokea. Ni kweli kwamba huenda mtu akaonelea miongoni mwa hekima ni kugeuza jambo fulani. Lakini sio kwa spidi tunayoitaka sisi. Jamii iko tofauti na ule wema ambao sisi tunawatakia. Katika hali hiyo ni lazima kwa mtu kwenda na watu katika kuwarekebisha kwa kuanzia na lile ambalo ni muhimu zaidi na kushuka. Kwa msemo mwingine aanze kurekebisha kile ambacho ni muhimu na cha haraka zaidi. Halafu aende na watu hatua baada ya hatua mpaka aweze kufikia malengo.

[1] 15:95

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017