15. Hadiyth “Jua halijapatapo kutua wala kuchomoza katika siku iliyo bora zaidi kuliko siku ya ijumaa… “

697- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jua halijapatapo kutua wala kuchomoza katika siku iliyo bora zaidi kuliko siku ya ijumaa. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa kinafazaika siku ya ijumaa isipokuwa vizito viwili: majina na watu.”

Ameipokea Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” zao pamoja na Abu Daawuud na wengineo kwa tamko lililo refu zaidi kuliko hili. Mwishoni mwake imekuja:

“Hakuna kiumbe chochote isipokuwa kinasikiliza kwa makini siku ya ijumaa tokea pale jua linapochomoza mpaka pale linapozama kwa sababu ya kuchelea Saa. Isipokuwa majini na watu ndio hawafanyi hivo.”[1]

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/437)
  • Imechapishwa: 12/01/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy