15. Faida nyingine ni lini mwanamke anajua kama damu yake imekauka

Mwanamke atajua vipi kwamba hedhi yake imekatika? Atalijua hilo kwa kukatika damu yake, jambo ambalo linapatikana kwa moja katika alama mbili:

Ya kwanza: Kushuka kwa maji meupe. Hayo ni maji meupe yanayofuatia hedhi. Maji hayo yanafanana na maji ya chokaa. Kuna uwezekano maji hayo yakawa na rangi isiyokuwa nyeupe. Huenda hali yake ikatofautiana kutegemea na hali za wanawake.

Ya pili: Ukavu kwa njia ya kwamba ataweka kitambara au pamba ndani ya tupu yake kisha akitoe hali ya kuwa ni kikavu na hakina kitu katika damu, rangi ya kijivu wala rangi ya manjano.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 31
  • Imechapishwa: 28/10/2019