15. Dalili ya kumi na tatu kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

14- Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah aliwaumba viumbe na akapanga mipango ambapo akawachukua watu wa upande wa kuume kwenye mkono Wake wa kuume na watu wa upande wa kushoto kwenye ule mwingine – na mikono Yake yote miwili ni ya kuume – kisha akasema: “Mimi siye Mola wenu?”[1]

Hadiyth ni nzuri na ameipokea Ibn Battwah katika “al-Ibaanah”.

[1] al-Ibaanah (227).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 20
  • Imechapishwa: 19/06/2019