15- Muhammad bin Ahmad bin Muhammad al-Jaaruudiy ametuhadithia: al-Husayn bin Muhammad bin Mukhaariq ametuhadithia Tastur: Yahyaa bin Mu´aadh al-Ghazzaal ametuhadithia: Yahyaa bin Ghaylaan ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wakiy´ bin Baziy ametuhadithia, kutoka kwa Rawh bin al-Qaasim: Suhayl bin Abiy Swaalih amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika du´aa yake:

“Wewe ni Uliye dhahiri; hakuna kitu juu Yako[1]. Wewe ni Uliyefichikana; hakuna kitu kinachojificha Kwako.”[2]

[1] Imaam ad-Dashtiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“4- Imaam Ismaa´iyl bin Muhammad bin al-Fadhwl al-Aswbahaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wanachuoni wamezungumzia kikomo/mpaka kwa ibara mbalimbali. Ufupi wa ibara hizo ni kwamba mpaka ni sehemu inayotenganisha na sehemu nyingine. Mwenye kusema kuwa Allaah hana mpaka na akawa anakusudia kuwa viumbe hawamzunguki kwa ujuzi wake, amepatia. Anayekusudia kuwa Allaah hajizunguki Mwenyewe kiujuzi ni mpotevu. Yule mwenye kukusudia kuwa Allaah yuko kila mahali kwa dhati Yake ni mpotevu pia.”

5- ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy – imamu wa mashariki – amesema:

“Jahmiyyah wanadai kuwa Allaah hana mpaka. Wanamaanisha kwa maneno haya kuwa Allaah si kitu. Viumbe wote wanajua hakuna kitu chochote kile isipokuwa kina mpaka na sifa…

Madhehebu ya Salaf ni kwamba Allaah ndiye wa mwanzo na wa milele. Ana mpaka ambao hakuna yeyote anayeujua isipokuwa Yeye tu, lakini asiwepo yeyote atayefikiria kuwa amekomeka Mwenyewe.”

6- Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake kwa ukamilifu Wake. Anajua na anasikia kutoka juu ya ´Arshi. Hakuna kitu katika viumbe Wake kinachofichikana Kwake, hakuna chochote kwao kinachofichikana Kwake. Yuko juu ya ´Arshi, amewazunguka kwa elimu Yake na anawaona.” (Ithbaat-ul-Hadd lil-Laah, uk. 105)

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Imethibiti kutoka kwa maimamu wa Salaf ya kwamba Allaah yuko na kikomo, ambacho Yeye peke yake ndiye ana ujuzi wake na kwamba ametengana na viumbe Wake. Ahl-ul-Hadiyth was-Sunnah wameandika vitabu juu ya hilo.” (Bayaan Talbiys-il-Jahmiyyah (03/590))

[2] Muslim (2713).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 37
  • Imechapishwa: 20/01/2017