15. Ameona damu kwa siku moja


Swali 15: Ni kipi anachotakiwa kufanya mwanamke katika kile kipindi amezowea kupata ada akiona damu kwa siku moja na siku ya kufuata asione damu mchana mzima?

Jibu: Dhahiri ni kwamba kusafika huku au ukavu huu aliopata katika masiku ya hedhi yake yanafuatia hedhi na hivyo haizingatiwi ni kutwahirika. Kujengea juu ya haya atabaki hali ya kujizuia kutokana na yale anayojizuia kwayo mwenye hedhi. Baadhi ya wanachuoni wengine wakasema kwamba yule ambaye siku za ada yake inafika siku anaona damu na siku nyingine anaona kukauka kwa damu, basi ile siku anaona hedhi itazingatiwa ni hedhi na ile siku anaona hedhi imekauka itazingatiwa ni kutwahirika mpaka ifikie siku kumi na tano. Zikishapita zaidi ya siku kumi na tano basi damu yenye kutoka baada ya hapo itazingatiwa kuwa ni damu ya ugonjwa. Haya ndio yaliyotangaa katika madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 16
  • Imechapishwa: 25/06/2021