15. Aina mbili za wanafunzi wenye kuhifadhi

Mwanafunzi! Tambua kuwa ubongo ni kama mtoto. Ukiuzoesha kuhifadhi utahifadhi na ukiuzoesha uzembe utazembea. Ubongo ni kama mtoto mchanga. Ukiufunza basi utaelimika na ukiuacha hautoelimika kitu. Hapa wanafunzi wamegawanyika sehemu mbili:

1- Baadhi ya wanafunzi hawajizoezi kuhifadhi hata siku moja.

2- Wengine wanataka kuhifadhi kiasi wasichokiweza.

Aina za watu wote wawili hawa hawafikii elimu yoyote.

Mwanafunzi anatakiwa kuufanyisha mazoezi ubongo wake. Aanze kwa kile anachokiweza kukihifadhi. Halafu baada ya hapo aende hatua baada ya hatua.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016