Download

22- Anatakiwa kusema mfano wa yale yanayosemwa na muadhini isipokuwa pale muadhini ataposema:

حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ وَحَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ

“Njooni katika swalah! Njooni katika mafanikio.”

Hapo aseme:

لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ

“Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”[1]

23- Wakati muadhini ataposema “ash-Haduu an laa ilaaha…. ” aseme:

وَأَنَا أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبَّاً، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولاً، وَبِالْإِسْلاَمِ دِينَاً

“Na mimi nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa pekee hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Nimeridhia Allaah kuwa Mola, Muhammad kuwa Mtume na Uislamu kuwa ndio dini yangu.”[2]

24- Anatakiwa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kumaliza kumuitikia muadhini[3].

25- Aseme:

اللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ، وَالصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ، آتِ مُحَمَّداً الْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ، وَابْعَثْهُ مَقَامَاً مَحمُوداً الَّذِي وَعَدْتَهُ

“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia, swalah iliosimama, mpe Muhammad wasiylah na fadhilah na mfikishe katika ngazi yenye kusifiwa ambayo Umemuahidi.”[4]

26- Ajiombee du´aa baina ya adhaana na kukimiwa swalah. Kwani du´aa kipindi hicho hairudishwi[5].

[1] al-Bukhaariy (01/152) nambari. (611) na (613), Muslim (01/288) nambari. (383).

[2] Muslim (01/290) nambari. 386.

[3] Muslim (01/288) nambari. (384).

[4] al-Bukhaariy (01/152) nambari. (614). ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) ameifanya nzuri cheni ya wapokezi wake katika “Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk. 38

[5] at-Tirmidhiy (3594) nambari. (3595), Abu Daawuud (525), Ahmad (12200). Tazama “Irwaa´-ul-Ghaliyl” (01/262).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 01/09/2018