149. Kuwapa pesa wafiwa wa maiti


Swali 149: Baadhi ya wale wenye kutoa rambirambi hutoa kitu katika pesa kuwapa wafiwa wa maiti kutegemea na uwezo wao. Je, kitendo hichi kinafaa[1]?

Jibu: Sunnah ni kuwatengenezea chakula kukiwa na wepesi wa kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofikiwa na khabari za kufa kwa Ja´far bin Abiy Twaalib siku ya Mu´tah alisema kuiambia familia yake:

“Watengenezeeni familia ya Ja´far chakula. Kwani hakika wamefikwa na kitu kinachowashughulisha.”[2]

Ni vizuri wakiwatengenezea chakula watachokula.

Kuhusu kuwapa pesa ni jambo halikusuniwa. Isipokuwa wakiwa ni mafukara na wahitaji. Hawa wasipewe wakati wa kutoa mkono wa polo. Lakini wapewe kipindi kingine kwa ajili ya umasikini na kuhitaji kwao.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/389).

[2] Ahmad (1754), Ibn Maajah (1610), at-Tirmidhiy (998) na Abu Daawuud (3132).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 108
  • Imechapishwa: 23/01/2022