149. Aina mbili za elimu ya dini na hukumu zake

Kuna sampuli mbili za kujifunza dini.

1- Sampuli ya kwanza: Faradhi kwa kila muislamu. Hakuna yeyote anayepewa udhuru kwa kutoyajua. Hayo ni yale ambayo dini ya mtu haiwezi kusimama isipokuwa kwayo. Kwa mfano kuijua ´Aqiydah sahihi, yanayokwenda kinyume nayo au kiupunguza, kuzijua hukumu za swalah, hukumu za zakaah, kuzijua hukumu za swawm, kuzijua hukumu za Hajj na ´Umrah. Kwa msemo mwingine zile nguzo tano za Uislamu. Haya ni lazima kwa kila muislamu mwanaume na mwanamke kujifunza nazo. Vinginevyo vipi ataitekeleza dini yake kwa njia ipasayo ikiwa hakujifunza nguzo tano hizi?

2- Fungu la pili: Ni yale ambayo kuyajua ni faradhi kwa baadhi ya watu na sio kwa kila muislamu. Bali ni kwa kwa yule mwenye uwezo wa kufanya hivo. Ni kujifunza milango mingine iliobaki ya elimu; kama mfano wa Fiqh ya biashara, Fiqh ya mirathi, Fiqh ya ndoa, Fiqh ya adahbu za Kishari´ah na mengineyo. Kujifunza mambo haya ni faradhi kwa baadhi ya watu. Ni lazima yawepo kwa sababu watu wanayahitajia. Lakini kukipatikana ambao watayasimamia uwajibu unakatika kwa wengine na inakuwa kwa haki ya wengine yamependekezwa na ni miongoni mwa mambo bora yaliyopendekezwa. Kwa sababu pengine kukawa hakuna uwezekano kwa kila mmoja kujifunza milango hii ya elimu. Kwa ajili hio ndio maana kujifunza nayo ikawa ni faradhi tu kwa baadhi ya waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 189-190
  • Imechapishwa: 13/03/2019