148. Wafiwa kuwaalika wageni kula pamoja nao


Swali 148: Wafiwa wa maiti wakitumiwa na watu chakula cha mchana au chakula cha jioni ambapo watu wakakusanyika juu yake nyumbani kwa maiti. Je, ni katika maombolezo yaliyoharamishwa?

Jibu: Hayo sio maombolezo. Kwa sababu hawakukitengeneza wao, bali wametengenezewa nacho. Ni sawa wakawaita wataokula pamoja nao katika kile chakula walichoagiziwa. Kwa sababu kinaweza kuwa kingi kinachozidi juu ya mahitaji yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 22/01/2022