148. Mahimizo ya Allaah na Mtume wake kujifunza dini

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekokoteza juu ya kujifunza elimu yenye manufaa na kuifanyia kazi. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

”Haiwapasi waumini watoke wote pamoja kwenda [vitani]. Hivyo basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao kundi moja wajifunze dini na ili wawaonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kujitahadharisha.” (at-Tawbah 09:122)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri, basi humpa ufahamu akaifahamu dini.”[1]

Kuwa na ufahamu katika dini na kujifunza elimu yenye manufaa ni katika alama zinazoonyesha kuwa Allaah anamtakia kheri mtu. Sambamba na hilo kupuuza kujifunza dini ni katika zinazoonyesha kuwa Allaah anamtakia shari mtu.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (71) na Muslim (1037).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 189
  • Imechapishwa: 13/03/2019