147. Kitenguzi cha kumi: Kuipuuza dini mtu hajifunzi nayo wala haifanyii kazi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

La kumi:

Kuipuuza dini ya Allaah kwa njia ya kwamba mtu hajifunzi nayo wala haifanyii kazi. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ

”Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayah za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi Tutawalipiza wahalifu.” (as-Sajdah 32 :22)

MAELEZO

Aayah ambazo zimefahamisha juu ya ukafiri wa yule mwenye kukengeuka ni nyingi. Kwa mfano maneno Yake (Ta´ala):

وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنذِرُوا مُعْرِضُونَ

”Wale waliokufuru wanapuuza yale wanayoonywa.” (al-Ahqaaf 46:03)

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ

”Ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyekumbushwa Aayah za Mola wake, akazipuuza na akayasahu yale iliyotanguliza mikono yake.” (al-Kahf 18:57)

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا

”Wanapoambiwa: “Njooni katika yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume, basi utawaona wanafiki wanakugeuka kwa upinzani.” (an-Nisaa´ 04:61)

وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ

”Anayejifanya kipofu na  Ukumbusho wa Mwingi wa rehema, basi Tunamwekea shaytwaan awe ndiye rafiki yake.” (az-Zukhruf 43:36)

وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا

”Anayepuuza Ukumbusho wa Mola wake, basi atamsukuma katika adhabu kali inayozidi.” (al-Jinn 72:17)

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ

”Utakapokufikieni kutoka Kwangu uongofu, basi atakayefuata uongofu Wangu hatopotea na wala hatopata mashaka. Atakayepuuza ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya Qiyaamah hali akiwa kipofu. Atasema: “Mola wangu! Mbona Umenifufua kipofu na hali nilikuwa nikiona?” Atasema: “Hivyo ndivyo zilikufikia Aayah Zetu ukazisahau   na kadhaalika leo umesahauliwa.” (Twaaha 20:123-126)

وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ انصَرَفُوا ۚ صَرَفَ اللَّـهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ

”Inapoteremshwa Suurah, basi wanatazamana wenyewe kwa wenyewe [kisha hunong’onezana]: “Je, kuna mmoja yeyote anayekuoneni?” Kisha wanageuka kuondokea mbali. Allaah amewagezua nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.” (at-Tawbah 09:127)

لَّا تَجْعَلُوا دُعَاءَ الرَّسُولِ بَيْنَكُمْ كَدُعَاءِ بَعْضِكُم بَعْضًا ۚ قَدْ يَعْلَمُ اللَّـهُ الَّذِينَ يَتَسَلَّلُونَ مِنكُمْ لِوَاذًا ۚ فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

”Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Allaah anawajua wale wanaoondoka kunyemelea kwa kujificha miongoni mwenu. Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake isije kuwapata fitina au wakapatwa na adhabu iumizayo.” (an-Nuur 24:63)

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametahadhariha katika Aayah hizi  kupuuzilia mbali Ukumbusho Wake; nayo ni Qur-aan na Sunnah. Kwa njia ya kwamba mtu hajifunzi navyo, havifanyii kazi kwa aina mbalimbali za matishio ya adhabu. Kando na hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekokoteza juu ya kujifunza elimu yenye manufaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 188-189
  • Imechapishwa: 13/03/2019