146. al-Qummiy upotoshaji wake wa tatu wa al-A´raaf


al-Qummiy amesema:

“Abul-Jaaruud amepokea kutoka kwa Abu Ja´far ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake:

وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ

“Wale wanaoshikamana barabara na Kitabu na wakasimamisha swalah, hakika Sisi hatupotezi ujira wa watendao mema.”[1]

“Imeteremshwa kuhusu kizazi cha Muhammad na wafuasi wao.”[2]

Aayah ni yenye kuenea na inawahusu wale wote wenye kushikamana na yale yaliyokuja na Mitume. Katika wao unaingia Ummah huu mtukufu – Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuifupisha kwa kizazi cha Muhammad ni katika kumsemea uongo mkubwa kabisa Allaah.

[1] 07:170

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/246).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 208
  • Imechapishwa: 19/09/2018