144. Kujifananisha na Ahl-ul-Bid´ah ni aina fulani ya kutoka katika Shari´ah ya Muhammad

Hali kadhalika yule atakayejifananisha nao katika baadhi ya mambo au katika mambo yao mengi, yote haya ni aina za kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kiwango chake. Ni wajibu kwa muislamu kushikamana na Qur-aan na Sunnah na kuitakidi kwamba vyote viwili vimekamilika, ni wenye kuenea, inasilihi katika kila zama na mahali na mtu asiwe na shaka yoyote au kusita katika jambo hilo. Hili ndilo la wajibu kwa waislamu daima na siku zote.

Ni kwamba kwamba baadhi ya mambo yanaweza kufichikana kwa baadhi ya watu na wasipate hukumu yake katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na upungufu wa ufahamu wao na sio kwa sababu ya upungufu katika Qur-aan na Sunnah. Vinginevyo ni kuwa lau wangelikuwa na elimu sahihi na ubobeaji basi wangelipata kwamba Qur-aan na Sunnah ndani yavyo kuna kila anachokihitajia mwanadamu mpaka kitaposimama Qiyaamah. Lakini yule ambaye hakubainikiwa na haya, basi ni juu yake aituhumu elimu na akili yake na wala asiituhumu Qur-aan na Sunnah na kusema kwamba ndani yake hakuna kitu kadhaa na kadhaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 184
  • Imechapishwa: 12/03/2019