144. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa nane wa al-A´raaf

al-´Ayyaashiy amesema:

“Abu Baswiyr amesema kuhusiana na maneno ya Allaah:

فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Basi wale waliomuamini na wakamtukuza na wakamnusuru na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.”[1]

“Abu Ja´far amesema: “Nuru ni ´Aliy.”[2]

Aayah hii tukufu ni dalili ya wazi kabisa juu ya yale waliyosimama kwayo Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale ambapo walimuamini yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakamtukuza, wakamnusuru nusura kubwa dhidi ya maadui zake, wakamuheshimu na wakamfuata na kushikamana na ile nuru na mwongozo aliokuja nao, nayo si nyingine ni hii Qur-aan:

نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ

“Ameiteremsha haya Roho mwaminifu.”[3]

Halafu Allaah akawashuhudia kufaulu duniani na Aakhirah.

Ndipo wakaja Raafidhwah Baatwiniyyah ambao wakapotosha makusudio ya Allaah ya nuru ambayo ilichukuliwa na Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakaifuata na wakaipachika kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Uhalisia wa mambo ni kwamba yeye si mwingine isipokuwa ni mmoja katika wale ambao waliongoka kwa nuru hii iliyoteremshwa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Asingeliifuata basi angeliangamia na asingelikuwa chochote.

Malengo ya Baatwiniyyah hawa ni kuwafanya watu wasiweze kuona ushahidi huu mkubwa na matapo kwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan ambayo ni nuru kutoka kwa Allaah; wanaongozwa kwayo wale walioongozwa na wanafaulu kwayo wale wenye kuifuata.

[1] 07:157

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/21).

[3] 26:193

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 204-205
  • Imechapishwa: 12/09/2018