143. Kuzusha katika dini ni aina fulani ya kutoka katika Shari´ah ya Muhammad

Hali kadhalika anaingia katika hiki yule ambaye anazua Bid´ah katika dini au akazua jambo jipya akidhani kuwa ni kheri na kwamba ni kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall), hii ni aina fulani ya kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu hawakutoshelezwa na yale aliyoweka Allaah (´Azza wa Jall) katika Shari´ah. Bali wakaona walete nyongeza na maana yake ni kwamba dini sio kamilifu na kwamba ina haja ya kuongezwa. Kwa ajili hii amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayefanya matendo yasiyoafikiana na amri yetu, basi itarudishwa mwenyewe.”[1]

Bi maana atarudishiwa mwenyewe.

“Tahadharini na mambo yaliyozuliwa! Kwani hakika kila kitachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotofu.”

Kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunajumuisha aina zote hizi. Lakini hata hivyo baadhi yazo ni khatari zaidi kuliko zingine. Kuna ambazo ni kuritadi, zengine ni upotevu na zengine ni kufuru ndogo. Yale waliyomo Suufiyyah waliopetuka mipaka ya kutoka katika Shari´ah nzima ni kufuru ya wazi.

[1] Ameipokea Muslim (18/1718) kupitia kwa ´Aishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 183-184
  • Imechapishwa: 12/03/2019