141. Miongoni mwa dalili kwamba Allaah atawafufua viumbe baada ya kufa II

Miongoni mwa dalili za kufufuliwa ni yale yanayoipitikia ardhi mimea kupata uhai. Wewe unaiona ardhi imekufa haina mmea hata mmoja kamee. Kisha Allaah anaiteremshia mvua. Halafu anaiteremshia mimea baada ya kwamba hapo kabla ilikuwa kame. Vivyo hivyo miili ardhini ilikuwa imehifadhiwa ndani ya ardhi ambapo Allaah akaiteremshia mvua. Kisha miili itamea na kukamilika. Kisha itapuliziwa roho. Nyinyi mnaona namna ardhi inavokuwa kame. Kisha inapata uhai kwa yale yaliyooteshwa juu yake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ndiye huipa ardhi uhai baada ya kufa kwake:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۚ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

”Miongoni mwa alama Zake ni kwamba utaona ardhi imetulia kame, kisha tunapoiteremshia maji inatikisika na huotesha. Hakika Yule aliyeihuisha, bila shaka ni Mwenye kuhuisha wafu, hakika Yeye juu ya kila kitu ni muweza.”[1]

Ambaye ameweza kuihuisha ardhi baada ya kufa kwake ni muweza wa kuihuisha miili baada ya kufa kwake. Kwa sababu viumbe vyote hivo vilikuwa hai baada ya kufa.

[1] 41:39

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 278-279
  • Imechapishwa: 16/02/2021