140. Mfumo wa uanasekula unaingia vilevile katika kichenguzi hiki

Kitenguzi hichi kunaingia vilevile uanasekula wenye kuona kwamba dini itenganishwe na nchi. Wanaona kuwa dini na ´ibaadah viwepo misikitini pekee. Ama biashara na hukumu mbalimbali kama za siasa wanaona kwamba hayaingii katika dini ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa ni watu wenyewe ndio wanahukumiana kwayo. Huu ndio mfuo wa uanasekula. Wanaona kuwa dini ni ya Allaah na nchi ni ya wote. Hawa wanaungana na wale Suufiyyah waliopindukia ambao wanaona kuwa wapo ambao wanaweza kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Upande mwingine wanasekula wanaona kuwa  mtu anaweza kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mambo ya siasa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 181-182
  • Imechapishwa: 11/03/2019