Allaah (Ta´ala) amesema:

يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ

Allaah anakutakieni mepesi – na wala hakutakieni magumu.”[1]

Aayah hii ni neema kutoka kwa Allaah juu ya Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mola wetu (Subhaanahu wa Ta´ala) anatujulisha kuwa anatutakia mepesi – na wala hatutakii magumu. Kama ilivyokuja katika Aayah nyingine:

وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ

“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[2]

Makusudio ya wepesi katika Aayah ni kwamba hukumu za dini ni sahali na nyepesi. Haikusudii yale yanayosemwa na baadhi ya watu wanaposema kuwa dini ni nyepesi na huku wanakusudia kutenda kila dhambi. Watu hawa wanataka kuiwepesisha dini kwa njia hii. Watu hawa ni wenye kukosea kosa kubwa. Haki ni kwamba dini hukumu zake ni sahali na nyepesi. Kitendo cha baadhi ya watu kuthubutu juu ya madhambi na kuacha faradhi na mambo ya wajibu ya Allaah kwa madai ya kwamba “dini ni nyepesi” ni jambo lisilokuwa na uhusiano wowote ule na Uislamu.

[1] 02:185

[2] 22:78

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 25-27
  • Imechapishwa: 02/06/2017