14. Unasemaje juu ya ambaye anaona uzito kujiita “Salafiy?”

Swali 14: Kuna vijana wanaona uzito kusema: “Mimi ni Salafiy.” Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Kwa nini wanaona uzito? Wanaona kujinasibisha na Salafiyyah ni jambo lina mapungufu? Hivi kweli mpaka mtu aweze kuhisi uzito ni jambo lenye kasoro kujinasibisha na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanachuoni, wasomi wa Fiqh, wasomi wa Hadiyth, wasomi wa Tafsiyr ya Qur-aan wenye kuwafuata – watu ambao wana ´Aqiydah sahihi katika kila zama na kila mahali wenye kufuata haki katika Qur-aan na Sunnah juu ya ufahamu wa wema waliotangulia (Salaf-us-Swaalih)? Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea.

Kwa yule ambaye anaangalizia mfumo wa Salaf ili ajaribu kuufuata na anasema kuwa yeye ni Salaf, mtu kama huyu kunatarajiwa juu yake kheri – Allaah akitaka. Ama ikiwa anaona uzito kutokana na sababu nyengine huenda akaadhibiwa kwa sababu ya kitendo hichi.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017