14. Ugaidi Saudi Arabia ulikuwepo tangu wakati wa mfalme ´Abdul-´Aziyz


Hii ni baadhi tu ya mifano ya ugaidi iliyozijaribu baadhi ya nchi za Kiislamu ikiwemo nchi yetu hii tukufu. Imepata sehemu yake vilevile tangu wakati mfalme ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdir-Rahmaan al-Fayswal Aal Su´uud aliposhika uongozi juu yake na kufanya umoja. Aliikufanya nchi kuwa na umoja kwa Tawhiyd na kutekelezwa kwa Shari´ah ya Allaah safi. Akasafisha aina zote za dhuluma na akaeneza sampuli zote za uadilifu. Baada ya Tawhiyd na faradhi zake alizofanya naona kuwa ndio jambo bora kabisa alilofanya. Hati ya kihistoria inathibitisha maneno yake pindi alipotuliza ulimwengu wa Kiislamu:

“Funguo za misikiti miwili mitakatifu ilianguka kwenye mikono aminifu. Tulitokomeza dhuluma na kueneza uadilifu nchini kote. Hakuna chochote tunachotamani kama waislamu wa ulimwengu kote kuja kwetu kuhiji. Njia zimefunguliwa. Hakuna yeyote atakayekudhuruni. Kuweni watulivu kikamilifu. Sisi wenyewe tutaenda Makkah kukutana na wale wajumbe wa Kiislamu na kuwakaribisha. Tumejikubalisha kuirudishia hajj mafanikio yake na enzi zake za kale.”

Halafu akasema (Rahimahu Allaah):

“Mimi, familia yangu, raia wangu na jeshi langu ni wanajeshi wa Allaah tunaopigania manufaa ya waislamu na mahujaji wanapewa dhamana ya usalama.”

Maneno haya mazuri yaliyohifadhiwa ambayo ni hati ya kihistoria yanazituliza nyoyo zinazopenda kheri na watu wa kheri na yanayabariki. Sambamba na hilo ni roketi ambazo kiongozi mwenye imani na mwenye ushujaa anazirusha kwa watu wenye nyoyo susuwavu na watu wenye nyoyo za dhuluma na za kipumbavu zinazotumbukia katika shari, dhuluma na ufisadi. Hawaingiwi wala na fikira ya kuwa wameshafariki hapa duniani na ni wala khasara hiyo siku ya Mwisho.

Mambo yakiwa namna hiyo, basi hakuna cha kushangaza kabisa kuona kunasheheni katika kisiwa cha Kiarabu usalama na amani na watu wake kuburudika na neema ya Uislamu na maisha mazuri tokea wakati huo mpaka pale Allaah atapotaka. Hii leo tunaona kikweli namna ambavyo msafiri anasafiri kutoka mashariki kwenda magharibi pasi na kumwogopa yeyote asiyekuwa Allaah. Himdi zote zinamstahikia Allaah. Tunamuomba atutunuku neema zaidi na atuondoshee matatizo.

Mfalme ´Abdul-´Aziyz ana haki ya kushukuriwa na kuombewa du´aa na kila raia wa kisaudi tangu hapo alipoifanya nchi kuwa na umoja mpaka pale watoto wake watukufu baada yake waliposhika kheri na ustawi unaoendelea mpaka hii leo na mpaka pale Allaah atapotaka:

´Adiy ameshika ukarimu wa baba yake

yule mwenye kumlinganisha mtu na baba yake hakudhulumu

Kiongozi na mfanya kazi wa misikiti miwili mitakatifu mfalme Fahd bin ´Abdil-´Aziyz amesema:

“Himdi zote zinamstahikia Allaah ambaye ametutunuku neema ya uhai na nchi yenye amani na Haram yenye amani na akajaalia usimamizi wa misikiti miwili mitakatifu, hajj, waswaliji na watembezi kuwa ni jukumu letu kubwa na tukufu zaidi.”

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 20-22
  • Imechapishwa: 14/04/2017