Miongoni mwa fadhilah za swawm ni kwamba itamwombea mwenye nayo siku ya Qiyaamah. ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Funga na Qur-aan vitamuombea mja siku ya Qiyaamah. Funga itasema:”Ee Mola Wangu! Nilimnyima chakula na matamanio. Hivyo nakuomba nikubalie maombi yangu kwake.” Qur-aan nayo itasema: “Nilimnyima kulala usiku. Hivyo nakuomba nikubalie maombi yangu kwake.” Awakubalie.”

Ameipokea Ahmad[1].

Ndugu wapendwa! Fadhilah za swawm hazifikiwi mpaka mfungaji atekeleze adabu zake. Hivyo jitahidini kuifanya vizuri funga yenu na chungeni mipaka yake na tubuni kwa Mola wenu kutokana na mapungufu yenu katika jambo hilo.

Ee Allaah! Tuchungie swawm zetu, utujaalie iweze kutuombea, utusamehe sisi na wazazi wetu na waislamu wote.

Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

[1] at-Twabaraaniy na al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh juu ya sharti za Muslim. al-Mundhiriy amesema:

”Wapokezi wake ni wenye kutumiwa kama hoja katika “as-Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 09/04/2020