14. Sifa ya nne ya mwanamke ili aweze kuitengeneza jamii

Sifa ya nne: Malezi mema.

Mwanamke awape watoto wake malezi mema. Watoto wake ndio wanaume wa mustakabali na wanawake wa mustakabali. Ile hatua ya kwanza ya ukuaji wanakutana na mama huyu. Mama huyu akiwa na maadili mema. Bali mama huyu akiwa ni mtu wa ´ibaadah, maadili mema na anatangamana na watu kwa wema na wakawa wamealeleka mikononi mwake, basi watakuwa na athari kubwa katika kuitengeneza jamii.

Kwa ajili hii ni wajibu kwa mwanamke aliye na watoto awatilie umuhimu watoto wake na atilie umuhimu suala la kuwapa malezi. Iwapo atashindwa kuwarekebisha basi atake msaada kutoka kwa baba yao au mlezi. Wataka msaada kutoka kwa mlezi wao wakiwa hawana baba. Mlezi huyu anaweza kuwa ndugu, wajomba, watoto wa kaka au wengineo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017